Majivu kwa ajili ya kuzuia mimba! Wanayalamba?
Baadhi ya wanawake wanaamini kwamba wakitumia njia za kisasa wanaweza kuharibu maumbile yao ya mwili ya asilia pamoja na kupata ulemavu. Wapo wanaoamini kuwa uzazi wa mpango upo kwa ajili ya kupunguza idadi ya watu kwa kuua mayai ya uzazi pindi watakapotumia dawa za kisasa kama kuchomwa sindano, kumeza vidonge, vipandikizi na kuwekewa kitanzi. Kutokana na kuamini njia za kisasa zina athari kwa afya zao, baadhi ya wanawake hususan waishio vijijini wanatumia majivu kama njia ya kuzuia kupata mimba. Hali hiyo imekuwa ikichochewa na waume zao kutowaruhusu kutumia njia za kisasa za uzazi wa mpango. Wapo wengine wanakoroga bluu na kunywa pindi wanapohisi wamepata mimba ikiwa ni imani ya kwamba mimba itaharibika. Wilaya ya Kishapu mkoani Shinyanga ina hospitali moja iliyopo Mwadui maeneo ya mgodini. Wilaya hii pia ina vituo vya afya vinne, zahanati 45 za Serikali na nne za watu binafsi. Wanawake katika vijiji vya Ilebelebe, Ikoma na Itilima...

Comments
Post a Comment