Posts

Showing posts from April, 2017

Madhara Ya Kula Mayai Yasipoiva Vizuri Kwa Afya

Image
Mayai ni moja ya vyakula vyenye viini lishe muhimu kwa ajili ya afya ya mwili wa binadamu. Kwa kawaida mayai kabla ya kuliwa, huandaliwa kwa njia mbalimbali ikiwa ni pamoja na kuchemshwa, kukaangwa au kuchanganywa na vyakula vingine kama vipande vya viazi mviringo ambavyo ni maarufu kwa jina la chips. Pia, kuna baadhi ya watu wanaopendelea kula mayai mabichi kama dawa ya tiba mbadala, kwa ajili ya kulainisha sauti na wengine hupendelea kula mayai ya kukaanga ambayo hayakukaushwa vizuri. Ukitembelea migahawa mingi utabaini kuwa watu wanakuwa na mitazamo tofauti na wanavyopenda kula mayai. Mfano kuna wanaoagiza watengenezewe mayai kwa mtindo unaojulikana kama ‘macho ya ng’ombe.’ Ukiagiza namna hiyo, mpishi atataka kuuliza kama ni ‘macho ya ng’ombe’ ya kugeuza. Ina maana kuwa ‘macho ya ngombe’ ya kugeuzwa ni yale yanayoivishwa pande zote lakini yale ambayo siyo ya kugeuza, huwa linaifa nusu. Upande mmoja unabaki ukiwa mbichi, na ndiyo raha ya baadhi ya watu. Hata ukienda kwa wa...

Mambo yanayofanya Mimba Yako Iwe Salama Zaidi

Image
KULINGANA na Hazina ya Umoja wa Mataifa ya Idadi ya Watu, zaidi ya wanawake nusu milioni hufa kila mwaka kutokana na matatizo yanayohusiana na mimba. Isitoshe, Shirika la Umoja wa Mataifa la Hazina ya Watoto linasema kwamba kila mwaka zaidi ya wanawake milioni 60 huugua vibaya wakiwa wajawazito hivi kwamba karibu thuluthi moja kati yao hupata majeraha au maambukizo yanayodumu maisha yote. Katika nchi zinazoendelea, wanawake wengi hupata mimba moja baada ya nyingine, hujifungua, na kujiachilia, jambo ambalo huwafanya wawe wachovu na wagonjwa. Naam, mimba inaweza kuleta madhara—hata kuhatarisha uhai. Je, mwanamke anaweza kufanya nini ili mimba yake iwe salama zaidi? Utunzaji wa Kiafya Kabla ya Kuwa Mjamzito Kupanga. Huenda waume na wake wakahitaji kuzungumza kuhusu idadi ya watoto ambao watapata. Katika nchi zinazoendelea, ni kawaida kuwaona wanawake wenye watoto wanaonyonya wakiwa wajawazito. Kwa kupanga vizuri na kutumia ufikirio unaweza kuruhusu wakati upite kabla ya mtoto mwingi...

Majivu kwa ajili ya kuzuia mimba! Wanayalamba?

Image
Baadhi ya wanawake wanaamini kwamba wakitumia njia za kisasa wanaweza kuharibu maumbile yao ya mwili ya asilia pamoja na kupata ulemavu. Wapo wanaoamini kuwa uzazi wa mpango upo kwa ajili ya kupunguza idadi ya watu kwa kuua mayai ya uzazi pindi watakapotumia dawa za kisasa kama kuchomwa sindano, kumeza vidonge, vipandikizi na kuwekewa kitanzi. Kutokana na kuamini njia za kisasa zina athari kwa afya zao, baadhi ya wanawake hususan waishio vijijini wanatumia majivu kama njia ya kuzuia kupata mimba. Hali hiyo imekuwa ikichochewa na waume zao kutowaruhusu kutumia njia za kisasa za uzazi wa mpango. Wapo wengine wanakoroga bluu na kunywa pindi wanapohisi wamepata mimba ikiwa ni imani ya kwamba mimba itaharibika. Wilaya ya Kishapu mkoani Shinyanga ina hospitali moja iliyopo Mwadui  maeneo ya mgodini. Wilaya hii pia ina vituo vya afya  vinne, zahanati 45 za Serikali na  nne za  watu binafsi.  Wanawake katika vijiji vya Ilebelebe, Ikoma na Itilima...

Health Effects of Cigarette Smoking

Cigarette smoking harms nearly every organ of the body, causes many diseases, and reduces the health of smokers in general. Quitting smoking lowers your risk for smoking-related diseases and can add years to your life Smoking and Death Cigarette smoking is the leading preventable cause of death in the United States. 1 Cigarette smoking causes more than 480,000 deaths each year in the United States. This is nearly one in five deaths. Smoking causes more deaths each year than the following causes combined: 4 Human immunodeficiency virus (HIV) Illegal drug use Alcohol use Motor vehicle injuries Firearm-related incidents More than 10 times as many U.S. citizens have died prematurely from cigarette smoking than have died in all the wars fought by the United States during its history. Smoking causes about 90% (or 9 out of 10) of all lung cancer deaths in men and women. More women die from lung cancer each year than from breast cancer. About 80% (or 8 out of 10) of all ...